728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 30, 2017

    BOURNEMOUTH YAMNASA BEKI WA CHELSEA KWA DAU LA REKODI


    London,England.

    Bournemouth imefumba macho na kumsajili beki wa kati wa Chelsea,Nathan Ake kwa dau la rekodi la £20m.

    Ake mwenye umri wa miaka 22  amejiunga na Bournemouth kwa mkataba wa miaka mitano na kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kununuliwa na klabu hiyo.

    Msimu uliopitaa,Ake anayetokea Uholanzi aliichezea Bournemouth kwa mkopo wa miezi sita na kuifungia mabao matatu kabla ya mwezi Januari kurejea Chelsea baada ya safu yake ya ulinzi kukumbwa na majeruhi.

    Ake anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Bournemouth katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Asmir Begovic aliyetokea Chelsea kwa dau £10m pamoja na Jermain Defoe aliyetokea Sunderland kwa uhamisho huru.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BOURNEMOUTH YAMNASA BEKI WA CHELSEA KWA DAU LA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top