728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 20, 2017

    USAJILI:Aliyedaiwa kuihujumu Kagera Sugar atua Mbeya City


    Mbeya,Tanzania.

    Mbeya City maarufu kama Wagonga Nyundo wameanza kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu na kombe la FA baada ya leo kumsajili beki wa kati wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi Mopa.

    Kyaruzi amejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa dau ambalo halijawekwa wazi.

    Msimu uliopita Kyaruzi pamoja na kipa wake Hussein Sharif ‘Casillas’ walisimamishwa na uongozi wa Kagera Sugar kwa tuhuma kuwa waliihujumu timu hiyo ilipocheza dhidi ya Yanga na kufungwa mabao 6-2 nyumbani CCM Kaitaba.

    Kyaruzi anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Mbeya City tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Juni 15.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Aliyedaiwa kuihujumu Kagera Sugar atua Mbeya City Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top