728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 22, 2017

    USAJILI:Monaco yachomoa mmoja kutoka Barcelona


    Monaco,Ufaransa.

    MABINGWA wa soka nchini Ufaransa,AS Monaco wameendelea kukiongezea makali kikosi chao kuhakikisha kinatetea ubingwa wake msimu ujao baada ya jana usiku kufanikiwa kumsajili winga wa kulia wa Barcelona,Jordi Mboula.

    Mboula mwenye umri wa miaka 18,zao la shule ya soka ya Barcelona,La Masia amejiunga na AS Monaco kwa mkataba wa miaka mitano utakaofikia mwisho Juni 2022.

    AS Monaco imeripotiwa kuilipa Barcelona fidia ya €3m ili kumnasa Mboula aliyegomea kusaini mkataba mpya baada ya kushindwa kuhakikishia namba kwenye kikosi cha wakubwa.

    Mboula anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na AS Monaco baada ya Youri Tielemans, Soualiho Meite, Jordy Gaspar pamoja na Diego Benaglio.

    Mwezi Februari mwaka huu Mboula aligonga vichwa vya habari vya michezo barani Ulaya baada ya kuifungia Barcelona bao maridadi kwenye mchezo wa michuano ya klabu bingwa Ulaya ya vijana dhidi ya Borussia Dortmund.

    Kabla ya kufunga bao hilo la juhudi binafsi Mboula aliwalamba chenga mabeki wote wa Borussia Dortmund.Bao hilo lilifanya aanze kufananishwa na staa mwenzake wa Barcelona,Lionel Messi.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Monaco yachomoa mmoja kutoka Barcelona Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top