728x90 AdSpace

Monday, June 19, 2017

ANAKUJA:Straika Ndanda anukia Jangwani


Omari Mponda kushoto


Dar Es Salaam,Tanzania.

STRAIKA wa Ndanda, Omari Mponda, amesema yupo mbioni kujiunga na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Yanga kama dili lake litakamilika.

Katika msimu uliopita, Mponda alionekana kuzisumbua Simba na Yanga ambapo alimaliza akiwa ameifungia klabu yake mabao sita.

Akizungumza jana, Mponda alisema kwa sasa bado anaendelea na mazungumzo na Yanga na mambo yakienda sawa atamwaga wino kwa kuitumikia katika mismu miwili.

“Sikuwa sawa mzunguko wa pili kutokana na majeraha ya goti, lakini naamini uwezo wangu niliouonyesha mzunguko wa kwanza umewavutia Yanga na ndio maana wameamua kuniita na kutaka mazungumzn na mimi,” alisema.

Alisema anaamini iwapo atajiunga na mabingwa hao na kupewa nafasi na mwalimu ataweza kutimiza malengo yake kwa kuwa mfungaji bora kutokana na kikosi cha Yanga kujaa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka.

CHANZO:BINGWA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: ANAKUJA:Straika Ndanda anukia Jangwani Rating: 5 Reviewed By: Unknown