728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 30, 2017

    REAL MADRID YAMPIGA BEI MTOTO WA ZIDANE


    Madrid,Hispania.

    REAL MADRID imeanza kuondosha watumishi hewa kwenye kikosi chake cha kwanza hii ni baada ya Jana usiku kumuuza kiungo wake,Enzo Zidane kwenda klabu ya Deportivo Alaves kwa ada ya uhamisho ambayo imefanywa siri.

    Enzo ,22, ambaye ni mtoto wa kwanza wa kocha, Zinedine Zidane amejiunga na Deportivo Alaves kwa mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha kurejea tena Real Madrid iwapo atahitajika hapo baadae.

    Enzo anaihama Real Madrid akiwa amefanikiwa kuicheza mchezo mmoja  pekee msimu uliopita tena ikiwa dhidi ya Cultural Leonesa kwenye mchezo wa kombe la mfalme ambapo alifunga bao moja. 

    Sehemu kubwa ya soka la Enzo limekuwa kwenye kikosi cha pili cha Real Madrid cha Castilla ambacho amekichezea michezo 78 na kufunga mabao saba. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID YAMPIGA BEI MTOTO WA ZIDANE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top