728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 20, 2017

    Mtibwa Sugar yamnasa Chuji wa Polisi Moro

    Hussein Iddi


    Morogoro,Tanzania.

    Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar kutoka Madizini,Manungu mkoani Morogoro wamefanikiwa kunasa saini ya wachezaji wawili waliofanya vyema katika timu zao msimu uliopita.

    Usajili uliofanywa na klabu ya wana tamtam ni mikakati ya kuboresha kikosi chake katika kuelekea msimu ujao, nyota waliosajiliwa hadi hivi sasa ni mshambuliaji matata kutoka katika timu ya Polisi Morogoro Salum Ramadhani Kihimbi maarufu “Chuji”.

    Nyota mwingine ni Hussein Idd aliyenaswa kutoka katika timu ya jeshi ya JKT Oljoro na anamudu kucheza nafasi ya beki wa kati.

    Nyota wote wawili wameingia kandarasi ya kuitumikia Mtibwa Sugar miaka miwili, Aidha mbali na nyota hao kocha mkuu Zuber Katwila kwa kushirikiana na benchi la ufundi wamesema watapandisha baadhi ya vijana kutoka katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar.

    Salum Ramadhani Kihimbi "Chuji"


    Uongozi wa Mtibwa Sugar unaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi hivyo basi usajili bado unaendelea na nyota wengine wanatarajiwa kuingia makubaliano na Mtibwa Sugar.

    Pia uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar unapenda kuwa taarifu wapenzi na mashabiki wake kuwa kuna baadhi ya nyota ambao mikataba yao imefikia tamati na klabu ya Mtibwa Sugar ,wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Jaffary Salum Kibaya , Said Mkopi, Maulid Gole “Adebayor”,Said Bahanuzi,Vicent Barnabas,Ally Lundenga na Ally Shomary.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mtibwa Sugar yamnasa Chuji wa Polisi Moro Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top