728x90 AdSpace

Wednesday, June 28, 2017

UTATA KWISHA:DONALD NGOMA ASAINI KANDARASI MPYA YA MIAKA MIWILI YANGA SC


Paul Manjale,Dar Es Salaam.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe,Donald Ndombo Ngoma hatimaye amemaliza utata wa timu ipi ataichezea katika msimu ujao wa soka hii ni baada ya mchana wa leo kusaini kandarasi mpya ya miaka miwili ya kuendelea kuwatumikia mabingwa watetezi wa ligi kuu bara,Yanga SC.

Ngoma ,27, ambaye alikuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kutimkia Simba SC pamoja na Polokwane City ya Afrika Kusini ameridhia kusaini kandarasi hiyo mpya baada ya kufikia makubaliano binafsi na Yanga SC ambayo imeonyesha nia ya kuendelea kuhitaji huduma yake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: UTATA KWISHA:DONALD NGOMA ASAINI KANDARASI MPYA YA MIAKA MIWILI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown