728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 29, 2017

    MALINZI,MWESIGWA WASOMEWA MASHITAKA 28,WAREJESHWA RUMANDE MPAKA JULAI 13


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    RAIS wa shirikisho la soka Tanzania,Jamal Malinzi pamoja na katibu wake mkuu Celestine Mwesigwa leo Alhamisi wamesomewa mashtaka 28 kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya jana kutiwa nguvuni na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa makosa ya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.

    Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia,

    Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee

    Na Mwisho ni shitaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375,418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsian

    Makosa hayo 28 yamewanyima haki ya kupata dhamana viongozi hao na badala yake wakataa rumande mpaka hapo Juni 13 ambapo kesi yao itasomwa tena.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MALINZI,MWESIGWA WASOMEWA MASHITAKA 28,WAREJESHWA RUMANDE MPAKA JULAI 13 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top