728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 27, 2017

    MONACO YAZIDI KUUZA NYOTA WAKE WALIOIPA UBINGWA


    Marseille,Ufaransa.

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa,Valere Germain (Pichani) akiwa ameshikilia jezi ya Marseille mara baaada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na timu hiyo akitokea Monaco kwa ada ya usajili ambayo haijawekwa wazi.

    Germain mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Marseille kwa mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vyake ya afya.

    Msimu uliopita Germain aliifungia Monaco mabao 10 na kuiwezesha timu hiyo ya Stade Louis II kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ligue 1 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000.

    Germain anakuwa mchezaji wa pili kuihama Monaco katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wa kwanza alikuwa ni Mreno Bernardo Silva aliyejiunga na Manchester City kwa ada ya £43m.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MONACO YAZIDI KUUZA NYOTA WAKE WALIOIPA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top