728x90 AdSpace

  • Latest News

      Wednesday, June 21, 2017

      USAJILI:Noti za Singida United zamnasa beki wa zamani wa Simba SC


      Paul Manjale,Dar Es Salaam.

      ALIYEKUWA beki wa zamani wa Simba SC,African Lyon na Coastal Union ya Tanga,Miraji Adam amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili.

      Miraji anayecheza nafasi ya beki wa kushoto amesaini mkataba huo leo mchana jijini Dar Es Salaam na kukabidhiwa jezi namba 4.

      Msimu uliopita beki huyo mzaliwa wa mkoani Morogoro alikuwa akiichezea klabu iliyoshuka daraja ya African Lyon aliyojiunga nayo baada ya kumaliza mkataba wake na Simba SC akitokea Coastal Union kwa mkopo.



      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Post a Comment

      Item Reviewed: USAJILI:Noti za Singida United zamnasa beki wa zamani wa Simba SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown