728x90 AdSpace

Thursday, June 29, 2017

BADO YUPO:TAMBWE ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC


Dar Es Salaam,Tanzania.

YANGA imeamua kuwabakisha mastaa wake walioipa ubingwa wa ligi kuu bara msimu uliopita baada ya jioni hii kumsainisha kandarasi mpya ya miaka miwili mshambuliaji wake tegemeo raia wa Burundi,Amisi Tambwe.

Tambwe aliyekuwa mapumzikoni nyumbani kwao Burundi amesaini kandarasi hiyo mpya baada ya ile ya awali kuwa imekwisha.

Tambwe anaungana na Mzimbabwe,Donald Ngoma ambaye jana pili alisaini kandarasi mpya ya miaka miwili ya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao mara tatu mfululizo za ligi kuu bara.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BADO YUPO:TAMBWE ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown