728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 16, 2016

    MBEYA CITY YAMTIA KIBURI KINNAH PHIRI

    Mbeya,Tanzania.

    Kocha Mkuu wa Mbeya City Fc Mmalawi Kinnah Phiri amesema sasa ana uhakika nyota wake wako kwenye kiwango kizuri
    kufuatia matokeo ya ushindi wa jumla ya bao 5 kwenye michezo miwili iliyopita kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inayoelekea ukingoni hivi sasa.

    Akizungumza na mbeyacityfc.com kocha Phiri ameweka wazi kuwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Coastal Union na ule wa 1-0 dhidi ya Mgambo JKT mwishoni mwa juma lililopita umempa  imani kubwa kuwa wachezaji wake sasa wameanza kuielewa vyema falsafa yake hasa kwa kuweza kufanikisha ushindi bila kuruhusu kufungwa bao katika michezo hiyo miwili.

    "Tulianza kucheza kwa mchezo wa kawaida sasa tumeongeza, tunacheza kwa spidi kubwa wachezaji wangu sasa wanajiamini kwa kiwango kikubwa tumefunga bao 5 bila kuruhusu kufungwa bao lolote, hili ni uhakika tosha kuwa kikosi changu sasa kiko imara kwenye ulinzi na pia kiko vizuri kwenye ufungaji, kwa sasa tuko kwenye mipango mizito kuhusina na mchezo ujao", alisema.

    Akiendelea  zaidi kocha huyo aliyewahi kuifundisha kwa mafanikio timu ya taifa ya Malawi alisema kuwa mara baada ya kurejea kutoka jijini Tanga kwenye mchezo dhidi ya Mgambo JKT alitoa siku chache za mapumziko kwa wachezaji wake na kuwataka kujiandaa kwa mazoezi yatakayoanza siku ya jumatatu tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu.

    "Baada ya Tanga, nilitoa mapumziko ya siku saba, vijana watarejea jumatatu tayari kwa mazoezi kabla ya kuivaa Mtibwa, nina imani siku saba zitatosha kuwaweka sawa kwa ajily ya mchezo huo, Sifahamu sana kuhusu timu hiyo ya Morogoro, kwenye ratiba  inaonyesha watacheza kesho ninaweza kufika kuwaona au nitatumia muda kuangalia mchezo wao kwenye TV, nataka kujua baadhi ya mambo muhimu ili nijiandae  vizuri kuweza kupata ushindi".


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAMTIA KIBURI KINNAH PHIRI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top