728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 19, 2016

    MIGI:AZAM FC BADO INA NAFASI SHIRIKISHO

    Tunis,Tunisia.

    Kiungo wa mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Jean Mugiraneza ‘Migi’,amesema kuwa licha ya timu hiyo kukabiliwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Esperance, bado ina nafasi ya kusonga mbele kwa kuwatoa waarabu hao na kutinga hatua ya 16 bora ya
    Kombe la Shirikisho Afrika.

    Azam FC tayari imewasili nchini Tunisia tokea juzi kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaofanyika
    leo Jumanne saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, wameingia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata awali jijini Dar es Salaam.

    Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz Migi alisema Azam FC ina wachezaji wengi wazoefu na wazuri jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri katika
    mchezo huo.

    “Nawajua Esperance,nimecheza nao mara nne nilipokuwa nacheza APR,
    mara zote nyumbani kwetu tulikuwa tunatoa nao sare au kushinda bao moja, lakini wamekuwa wakitufunga kwao,wanapocheza nyumbani
    wanapenda sana kumiliki mpira kwa kucheza pasi na pia waamuzi mara
    nyingi walikuwa upande wao kuwapendelea,” alisema.

    Migi alisema wanatakiwa kuwa makini sana katika mchezo huo kwa kukabiliana na presha kutoka kwa wapinzani wao ili waweze kupata matokeo wanayohitaji.

    Kiungo huyo kutoka Rwanda tokea ajiunge na Azam FC Julai mwaka jana,
    amekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo kwenye eneo la kiungo wa ukabaji, akiwa na uwezo wa kucheza mipira ya juu na ya chini pamoja na kutibua mashambulizi ya timu pinzani.

    Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB inahitaji sare yoyote au ushindi
    ili iweze kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora (play off), itakapokutana na moja ya timu iliyotoka kwenye hatua hiyo ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikifuzu hapo itatinga moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo (robo fainali).


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MIGI:AZAM FC BADO INA NAFASI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top