728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 21, 2016

    BARCELONA YAANZA TENA KUTUMBUA MAJIPU,YAINYUKA DEPO 8-0,SUAREZ APIGA NNE PEKE YAKE

    Coruna,Hispania.

    Baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu mfululizo ya Ligi ya La Liga hatimaye Barcelona imerejea tena katika makali yake ya kutoa vipigo vizito vizito baada ya Jumatano usiku kuichapa Deportivo La Coruna mabao 8-0 ugenini huko Riazor,La Coruna.

    Shujaa wa mchezo wa jana alikuwa na mshambuliaji Mruguayi Luis Suarez aliyefunga mabao manne na kutengeneza mengine matatu.

    Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi, Neymar, Mark Bartra na Ivan Rakitic.

    Ushindi huo muhimu umeifanya Barcelona iendelee kubaki kileleni na pointi zake 79.Katika mchezo mwingine Atletico Madrid imeifunga Athletic Bilbao bao 1-0 shukrani kwa bao la dakika ya 38 la mshambuliaji Fernando Torres.Atletico pia imefikisha pointi 79.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCELONA YAANZA TENA KUTUMBUA MAJIPU,YAINYUKA DEPO 8-0,SUAREZ APIGA NNE PEKE YAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top