728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 23, 2016

    EPL:MAN CITY YAIFANYIA MAUAJI STOKE CITY YAIPIGA 4-0 ETIHAD SASA IKO NAFASI YA TATU



    Manchester,England.

    Mabao mawili ya kinda Mnigeria Kelechi Ihenaicho na mengine ya Fernando Reges na Sergio Aguero yameiwezesha Manchester City kutoka kifua mbele nyumbani Etihad baada ya kuichapa Stoke City kwa mabao 4-0 katika mchezo mkali wa Ligi kuu England uliopigwa mchana wa leo.

    Manchester City ilianza kuandika bao la kuongoza dakika ya 35 tu ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Fernando Reges.Fernando alifunga bao hilo kwa kichwa akimalizia krosi safi ya winga Jesus Navas.Dakika ya 43 Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la pili kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Kelechi Iheanacho kuangushwa kwenye eneo la hatari.
     
    Dakika ya 64 Kelechi Iheanacho aliifungia Manchester City bao la tatu kabla ya kuongeza la nne dakika ya 74.Kufuatia ushindi huo Manchester City imefanikiwa kurejea nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 64 na kuishusha Arsenal mpaka nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 63.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EPL:MAN CITY YAIFANYIA MAUAJI STOKE CITY YAIPIGA 4-0 ETIHAD SASA IKO NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top