Regina Mary Nlodvu anasema alikuwa akicheza katika bustani yake, mbele ya nyumba wakati aliponyanyaswa kingono kwa mara ya kwanza na mwanamume ambaye aliyekuwa anamuamini.
"Alinipa pipi na kuniomba niketi kwenye paja lake," anakumbuka. "Na nilipofanya hivyo, alinyoosha mkono wake na kunyenyua nguo zangu na kuninyanyasa."
Regina anasema hii ilikuwa mara ya kwanza kunyanyaswa kingono - akiwa na umri wa miaka minane - lakini haikuwa mara ya mwisho.
Anasema mwanamume huyo huyo alirudi nyumbani kwake Ennerdale, Afrika Kusini, kwa kisingizio cha kuwatembelea wazazi wake na kumnyanyasa kingono na kumbaka mara nyingi zaidi katika miaka iliyofuata.
0 comments:
Post a Comment