728x90 AdSpace

  • Latest News

      Friday, July 31, 2015

      STAND UNITED KUTISHA VIBAYA MSIMU UJAO, TAZAMA PICHA YA JEZI ZAO MPYA HAPA






      Baada ya kupata mkataba mnono kutoka katika kampuni ya Acacia, timu ya Stand United inategemea kufanya vizuri sana msimu ujao na hivyo kuongeza jopo la ushindani wa vilabu pamoja na Azam Fc na wenda wakasitisha kile kilichozoeleka kwamba Simba na Yanga 
       ndizo zilizokuwa na uwezo wa kutwaa taji la Ligi Kuu kwa kupokezana kama sio timu moja wapo kutwaa mara mbili mfululizo.Hali hii haikutokana kwa sababu ya ukubwa wa vilabu, hali hii haikutokana kwa sababu ya kuwa na mashabiki wengi ila ukweli ni  vilabu vingi vilikuwa vikikumbwa na tatizo la kifedha mfano msimu mmoja nyuma tuliwahi kusikia maisha na mazingira mabovu waliokuwa wanaishi wachezaji wa Stand United kitu ambacho kingeweza kuwa kigumu kuleta ushindani kwa Yanga, Simba na Azam FC. Baada ya kampuni ya ACACIA inayojishughulisha na masuala ya uchimbaji wa madini kuidhamini klabu ya Stand United, yameanza kutokea mabadiliko chanya kiasi kwamba msimu ujao inawezekana Stand United ikafanya vizuri. Baada ya kumleta kocha wa kifaransa Patrick Liewig kuinoa klabu yao, July 30 imeonyesha aina ya jezi za kisasa itakazotumia msimu ujao.

      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Post a Comment

      Item Reviewed: STAND UNITED KUTISHA VIBAYA MSIMU UJAO, TAZAMA PICHA YA JEZI ZAO MPYA HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown