Dar Es Salaam,Tanzania.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,wameitoa nishai Majimaji FC ya Songea baada ya jioni ya leo kuichapa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Deus Kaseke dakika ya 19 na Amissi Tambwe aliyefunga mabao mawili dakika za 79 na 85.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa huko Sokoine,Mbeya,Azam FC imechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.
0 comments:
Post a Comment