London,Uingereza.
BAO la mkwaju wa penati lililofungwa na kiungo, Santiago Cazorla dakika ya 93 limeipa Arsenal ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ngumu ya Southampton katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Emirates,London.
Southampton ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 18 baada ya kipa wa Arsenal,Peter Cech,kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa faulo uliopigwa na Dusan Tadic.
Laurent Koscielny aliifungia Arsenal bao la kusawazisha kwa tiki taka dakika ya 29 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko,Arsenal iliwaingiza Alexis Sanchez,Olivier Giroud na Alex Iwobi kuchukua nafasi za Theo Walcott,Alex Chamberlain na Lukas Perez.Southampton walimtoa Jay Rodriguez na Dusan Tadic na kuwaingia Ward Prowse na Shane Long.
Mabadiliko hayo yaliinufaisha Arsenal kwani dakika ya 93 ilipata penati baada ya Olivier Giroud kufanyiwa madhambi ndani ya boksi na beki Jose Fonte na Santiago Cazorla kufunga bao la ushindi.
0 comments:
Post a Comment