Liverpool,Uingereza.
MAJOGOO Liverpool leo wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Anfield baada ya kuwachapa mabingwa watetezi wa ligi kuu England, Leceister City,kwa mabao 4-1 katika mchezo mkali na wa kuvutia uliochezwa huko jijini Liverpool.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Craig Pawson na kushuhudiwa na watazamaji 53075 ilishuhudiwa mabao ya Liverpool yakifungwa na Roberto Firmino aliyefunga mara mbili,Sadio Mane na Adam Lallana.
Bao la kufutia machozi la Leceister City limefungwa na Mshambuliaji wake mahiri Jamie Vardy.
0 comments:
Post a Comment