Dar Es Salaam,Tanzania.
KOCHA Msaidizi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,Juma Mwambusi,amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuishangilia timu hiyo mwanzo mwisho katika michezo yake mbalimbali ya ligi kuu.
Mwambusi amesema mashabiki wa Yanga SC wanapaswa kuiunga mkono timu yao kipindi chote cha mchezo badala ya kusubiri mabao yafungwe ndipo washangilie.
Mwambusi ameongeza kuwa sapoti ya mashabiki ndiyo kila kitu katika mchezo wa soka.Timu inapokuwa inashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao hupata nguvu ya ziada hata katika nyakati ngumu.
Wakati huohuo Mwambusi amewataka pia mashabiki wa Yanga SC kuendelea kumpa muda zaidi mshambuliaji wao mpya raia wa Zambia,Obrey Chirwa,ambaye mpaka sasa ameshindwa kuwika ndani ya kikosi chao.
Mwambusi amesema kuwa mashabiki wa Yanga SC wanapaswa kuendelea kumvumilivu Chirwa kwani ni mchezaji mzuri sana na muda siyo mrefu atakaa sawa.
"Siyo lazima mchezaji afunge bao ndipo aonekane amecheza".Amesisitiza Mwambusi.
0 comments:
Post a Comment