728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 08, 2016

    NYOTA WA ZAMANI WA TAIFA STARS AFARIKI DUNIA


    Morogoro,Tanzania.

    Mohamed Hussein Burhan, maarufu kama Mohamed Msomali,74, amefariki Ghafla Morogoro Mchana wa leo kwa tatizo la kifua.

    Marehemu amepata kuchezea Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania kwa Mafanikio makubwa kiasi cha kuimbwa na Marehem Mbaraka Mwinsheh Mwaruka katika ule wimbo Maarufu wa FAT NA TIMU YA TAIFA.

    Pia amepata kuchezea Timu ya Soka ya Mkoa wa Pwani wakati huo ikiunganisha Dar na Pwani,kabla ya kuwa Kocha wa Pan Africa ya Dar,Tumbaku na Reli za Morogoro na kustaafu na kuamua kuwa Khamsa Salawat... Wadogo zake wawili kwa Baba Mmoja, Marehem

    Hassan Msomali na Abdi Msomali nao pia walipata kuwika katika Soka la Morogoro.

    Allah ampe Kauli Thabiti... Aaamin...

    CHANZO:TBC TAIFA


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA WA ZAMANI WA TAIFA STARS AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top