Nairobi,Kenya.
KENYA itakuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji pamoja na ile ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame Cup.Hii ni kwa mujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),Nicholas Musonye.
Musonye amesema michuano ya Chalenji kwa wakubwa itapigwa mwezi Novemba mwaka huu huku michuano ya Kagame ikipangwa kufanyika mwezi Disemba.
Michuano ya kombe la Kagame ilikuwa ifanyike Dar es Salaam,Tanzania kati ya Juni na Julai lakini ilishindika baada ya shirikisho la soka la Tanzania,TFF,kudai kuwa lilikuwa limebanwa na ratiba ya timu ya taifa na vilabu vyake vya Yanga SC na Azam FC ambavyo vilikuwa vinashiriki michuano ya Afrika.
Katika michuano ya mwaka huu ya kombe la Kagame,Kenya, itawakilishwa na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchi hiyo,Gor Mahia na Ulinzi Stars ambayo ilishika nafasi ya pili msimu uliopita.
Aidha Musonye ameongeza kuwa Kenya inaweza kupata fursa ya kuwakilishwa na vilabu vitatu lakini hiyo itategemea mwitikio wa vilabu waalikwa.
0 comments:
Post a Comment