Nyon,Uswisi.
SHIRIKISHO la vyama vya soka ulimwenguni,FIFA,limetangaza kuvifungia vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid kutofanya usajili wa wachezaji wapya kwa kipindi cha misimu miwili.
Hatua hiyo ya FIFA imekuja baada kamati yake ya maadili kuzitupilia mbali rufaa zilizokatwa na vilabu hivyo ambavyo mapema mwaka huu vilikutwa na hatia ya kufanya udanganyifu katika masuala ya usajili wa wachezaji vijana wa kutoka nje ya Hispania.Zimevunja kanuni za 5, 9, 19 na 19 za usajili.
Hii ina maana kwamba vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid havitaruhusiwa kufanya usajili wowote ule wa wachezaji wapya mpaka mwaka 2018.
Aidha FIFA pia imetangaza kuvilima faini vilabu hivyo. Atletico Madrid imelimwa faini ya Pesa za Uswisi (Swiss francs) 900,000 ambazo ni sawa na Paundi 622,000).Real Madrid imelimwa faini ya Pesa za Uswisi (Swiss francs) ambazo ni sawa na 360,000 (£249,000).
Mwaka 2014 adhabu kama hii iliikumba pia klabu ya Barcelona.
0 comments:
Post a Comment