Abuja,Nigeria.
BAO alilofunga straika kinda wa Nigeria,Kelechi Iheanacho,Jumamosi iliyopita katika mchezo wa mwisho wa kundi G wa kuwania tiketi ya michuano ya AFCON 2017 dhidi ya Taifa Stars limechaguliwa kuwa bao bora la wiki na kituo cha Televisheni cha CNN.
Iheanacho,19,alifunga bao hilo dakika ya 77 baada ya kufumua mkwaju mkali wa mita 25 uliomshinda kasi kipa wa Taifa Stars,Aishi Manula,na kuipa Nigeria ushindi wa bao 1-0 huko Akwa Ibom Stadium,Uyo- Nigeria.
Bao hilo limeibuka kidedea baada ya CNN kulipambanisha na mabao yote yaliyofungwa katika michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ile ya kufuzu kombe la dunia kwa ukanda wa Amerika Kusini na Ulaya.
0 comments:
Post a Comment