London,Uingereza.
KIUNGO wa zamani wa Arsenal,Mfaransa Mathieu Flamini,amerejea ligi kuu kwa mlango wa nyuma baada ya leo hii kujiunga na Crystal Palace kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa kama mchezaji huru.
Falmini,32,amejiunga na Crystal Palace baada ya klabu yake ya zamani ya Arsenal kugoma kumpa mkataba mpya wa kuendelea kubaki Emirates.
Akiwa na Arsenal, Flamini,alifanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo 247 huku akiisaidia kutwaa ubingwa wa kombe la FA mara tatu.
0 comments:
Post a Comment