Cairo,Misri.
STRAIKA wa DR Congo,Kabongo Kasongo,(Pichani Kushoto),akitabasamu kwa furaha baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu ya Ittihad ya Misri ambayo mwishoni mwa mwezi Agosti ilimtupia virago Straika wa Cameroon,Samuel Nlend,23,baada ya kubaini kwamba ni mwathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Kasongo mwenye umri wa miaka 22,amejiunga na Ittihad akitokea klabu ya AS Kaloum ya nchini Guinea.
Samuel Nlend aliyetupiwa virago.
Akiongea baada ya kukamilika kwa uhamisho huo,Islam Serageldin,ambaye ni wakala wa Kasongo,amesema mteja wake anafuraha kubwa kutua Ittihad.Kinachofuata ni kufunga tu mabao yatakayoiwezesha timu hiyo kutimiza ndoto zake.
0 comments:
Post a Comment