728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 09, 2016

    PACHA YA MAVUGO,AJIB YAMTISHA LYANGA,AAMUA KUTIMKIA UMANGANI


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    KAMA unadhani pacha ya Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib ni tishio kwa timu pinzani pekee basi andika umeumia.Ukweli ni kwamba pacha hiyo ni tishio hata ndani ya Simba SC.

    Ishu iko hivi straika mrefu wa wekundu hao wa Msimbazi,Danny Lyanga, ameondoka jana nchini na kutimkia nchini Oman kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki katika klabu ya Oman Club inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza nchini humo.

    Akithibitisha kuondoka kwa straika huyo,Msemaji wa Simba SC,Haji Manara,amesema Lyanga amepata baraka zote toka kwa viongozi wa Simba SC na iwapo atafuzu wao kama klabu wapo tayari kumuuza.Simba SC haipo kwa ajili ya kuzuia mafanikio/ndoto za mchezaji yoyote yule.

    Lyanga ameamua kwenda kujaribu bahati yake nchini Oman baada ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza hata kwa dakika moja katika kikosi cha kwanza cha Simba SC ambacho kwa sasa macho yake yote yapo kwa pacha ya Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib na kwa mbali kuna Muivory Coast,Fredrick Blagnon.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PACHA YA MAVUGO,AJIB YAMTISHA LYANGA,AAMUA KUTIMKIA UMANGANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top