Mbeya,Tanzania.
Kocha Mkuu wa Mbeya City,Mzambia Kinnah Phiri, amesema hayupo tayari kupoteza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Azam FC, ambao watacheza kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine,Mbeya.
Phiri amesema kuwa anajua kama huo ni mchezo mkubwa kwao lakini lengo lake ni kuendeleza wimbi la ushindi ambalo litazidi kuwaweka kwenye nafasi nzuri ya kuongoza ligi.
“Nataka kulipa kisasi msimu uliopita walitufunga hapa nyumbani, msimu huu nisingependa kitu kile kitokee kwasababu tuna timu nzuri na mchezo huu umekuja tukiwa kwenye ari baada ya kufanya vizuri mechi tatu za awali”.Amesema Phiri.
Kuelekea mchezo huo kocha Phiri ametoa mapumziko ya siku tatu kwa wachezaji wake ili waweze kupumzika na kumaliza uchovu wa safari ndefu kujiandaa na mchezo huo wa ligi ya Vodacom.
CHANZO: GOAL
0 comments:
Post a Comment