London,Uingereza.
MENEJA wa muda wa Hull City,Mike Phelan na winga wa Manchester City,Raheem Sterling,kwa pamoja leo wametangazwa washindi wa tuzo yameneja na mchezaji bora wa mwezi Agosti wa ligi kuu England.
Phelan, 53,ameibuka mshindi mbele ya mameneja Jose Mourinho,Pep Guardiola na Antonio Conte baada ya kuipa Hull City ushindi katika michezo miwili kati ya mitatu ya mwanzo.
Tuzo ya bao bora la mwezi Agosti imekwenda kwa mshambuliaji wa Middlesbrough,Cristhian Stuani,bao hilo ni lile la mita 25 alilolifunga dhidi ya Sunderland.
0 comments:
Post a Comment