BAYERN Munich imeendeleza ubabe wake kwa Shalke 04 baada ya usiku huu kuichapa kwa mabao 2-0 katika mchezo pekee wa Bundesliga uliochezwa Ijumaa ya leo huko Veltins Arena.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi,Manuel Graefe,Bayern Munich ilijipatia bao lake la kwanza dakika ya 81 kupitia Robert Lewandowski baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Javi Martinez.
Bao la pili la Bayern Munich limefungwa na Joashua Kimmich dakika ya 90 baada ya kazi nzuri ya Robert Lewandowski.
Aidha katika mchezo huo mwamuzi,Manuel Graefe,alitoa kadi saba za njano.Kadi mbili zikienda kwa wenyeji Shalke 04 na tano kwa wageni Bayern Munich.
Ushindi huo umeifanya Bayern Munich ikae kileleni mwa msimamo wa ligi ya Bundesliga baada ya kufikisha alama sita kufuatia kushuka dimbani mara mbili.
0 comments:
Post a Comment