Paris, Ufaransa.
Paris Saint-Germain imeendelea kuonyesha kuwa maisha hayako sawa tangu ilipoondokewa na mshambuliaji wake wa zamani,Zlatan Ibrahimovic,hii ni baada ya usiku huu kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na AS Saint-Etienne nyumbani Parc des Princes.
Paris Saint-Germain ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya dakika ya 61 Lucas Moura kufunga kwa mkwaju wa penati.
Lakini bao hilo halikusaidia kitu kwani dakika ya 90,Robert Beric,aliyekuwa ametokea benchi aliifungia AS Saint-Etienne bao la kusawazisha na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment