728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 09, 2016

    BARCA KUISHTAKI SANTOS KWA KUCHEZEWA RAFU KATIKA USAJILI WA GABIGOL

    Barcelona, Hispania.

    BARCELONA imesema kuwa itaifungulia mashitaka klabu ya Santos ya Brazil kwa kukiuka makubaliano yao juu ya usajili wa mshambuliaji,Gabriel Barbosa 'Gabigol' aliyehamia Inter Milan ya Italia hivi karibuni.

    Akithibitisha taarifa hiyo Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona,Albert Soler, amedai klabu yake imechezewa rafu katika usajili wa mshambuliaji huyo ambaye mwezi uliopita aliisaidia Brazil kutwaa ubingwa wa Olimpiki.

    Nyaraka zilizovuja zimeonyesha kuwa mwaka 2013 Barcelona ilisaini makubaliano ya awali na Santos kuwa ikiwa Gabigol,20,atawekwa sokoni basi ipewe taarifa siku tatu kabla ili iweze kuona kama itaweza kufikia dau ambalo litakuwa limeletwa na klabu nyingine.  

    Lakini Barcelona imelalamika kuwa ilipewa siku moja tu ya Agosti 29 kuamua kama ingeipiku ofa ya £29m iliyokuwa imeletwa na Inter Milan.

    Gabigol alijiunga na Inter Milan siku ya mwisho ya usajili barani Ulaya ambayo ilikuwa ni Agosti 31 baada ya kuitumikia Santos kwa miaka minne.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA KUISHTAKI SANTOS KWA KUCHEZEWA RAFU KATIKA USAJILI WA GABIGOL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top