728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 09, 2016

    HII HAPA TAARIFA JUU YA AFYA YA MALIMI BUSUNGU

    Dar es salaam,Tanzania.

    MSHAMBULIAJI wa Yanga, Malimi Busungu hataonekana tena uwanjani labda hadi timu yake itinge robo fainali ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho baada ya juzi Jumamosi kuumia kwenye paji la uso na mbavu.

    Busungu aliumia wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa baada ya kugongana na kipa Yuri Jkose na nafasi yake ilichukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

    Kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Edward Bavu, Busungu alikimbizwa Hospitali ya Temeke na alilazwa kutokana na kusikia maumivu ya mbavu na jana asubuhi aliruhusiwa akiwa amepigwa nyuzi nne kwenye paji la uso.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII HAPA TAARIFA JUU YA AFYA YA MALIMI BUSUNGU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top