728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 09, 2016

    MSIBA!!MCHEZAJI MWINGINE AFIA UWANJANI BRAZIL

    Minas Gerais,Brazil.

    Ikiwa bado dunia inaomboleza kifo cha kiungo wa Cameroon Patrick Ekeng aliyefariki Ijumaa wakati akiichezea klabu yake ya Dinamo Bucuresti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Romania, habari nyingine mbaya imeripotiwa kutoka nchini Brazil.

    Taarifa zinasema kiungo wa nchi hiyo Bernardo Ribeiro amefariki dunia jana Jumapili kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mshituko wa moyo.

    Ribeiro,26 aliyekuwa akiicheza klabu moja ya ridhaa ya huko kwao Minas Gerais inadaiwa ghafla alianza kujisikia vibaya na kudondoka chini.Alikimbizwa katika hospitali ya jirani ya Sao Sebastiao lakini alipofikishwa madaktari waligundua tayari alikuwa ameshafariki.

    Kabla ya kifo chake Ribeiro alifanikiwa kuvichezea vilabu vya Friburguense,Flamengo na kisha kwenda Albania kuchezea klabu ya Skenderbeu Korce,Newcastle Jets ya Australia, pamoja na katika mataifa ya Italia na Finland

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MSIBA!!MCHEZAJI MWINGINE AFIA UWANJANI BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top