728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Kocha Oliver , Simba mpeni muda Mavugo Mtafurahi



    Farid Miraji,Dar Es Salaam.

    KOCHA mkuu wa Burundi ,Alain Oliver Niyungeko ampigia saluti mshambuliaji hatari wa Simba Fc Laudit Mavugo huku akisema wampe muda ili wavune  matunda mazuri  kutoka kwa nyota huyo. Mavugo ambae siku za hivi karibuni ameonyesha ni mchezaji mwenye kipaji cha pekee licha  kuanza vibaya kwenye msimu wa kwanza huku baadhi ya watu wakimponda kwa kutokuwa na msaada na timu yake.

    Kocha Niyungeko akiongea kutoka Burundi "Kwa Huku  nyumbani Burundi Mavugo ndiye mshambuliaji tishio, licha ya huko Tanzania  Amissi Tambwe kuwa ndiyo mkali wa mabao huku akiwa na rekodi ya kuchukua mfungaji bora katika msimu miwili" alisema Alain Oliver Niyungeko 

    Mavugo ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, aliwahi kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Burundi hata kwenye timu ya taifa amekua akifanya vizuri hivyo basi Simba wamtumie vizuri katika safu ya ushambuliaji na amini atakuwa tishio Tanzania Kama Tambwe.

    Aidha "kocha huyo amekuwa akikunwa na kiwango cha mshambuliaji huyo ambae amekuwa kama lulu katika soka la burundi huku akiwapongeza Simba kwa kunasa kifaa hicho".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kocha Oliver , Simba mpeni muda Mavugo Mtafurahi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top