728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Cannavaro:Kwa juhudi zetu tutafuzu


    Farid Miraji,Dar Es Salaam,

    MARA baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 juzi Jumamosi dhidi ya MC Alger kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika,nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro' amesema licha ya wapinzani kuwa wagumu lakini bado wana nafasi ya kufuzu hatua inayofuata. 

    Akizungumzia mipango yao kuelezea mchezo wa marudiano utakaochezwa wikendi ijayo huko Algers,Cannavaro amesema watajitahidi kucheza vizuri kwa maelekezo ya mwalimu ili waweze kulilinda bao lao moja na wakipata nafasi ya kushambulia watawafunga la pili.

    "Tukiwa ugenini huwa tunacheza vizuri na kuonyesha kandanda safi. Kwangu mimi sina wasiwasi na ninaamini lolote linawezekana kwa juhudi zetu tutafuzu" alisema Cannavaro.

    Aidha mchezaji huyo amezungumzia kuhusu kuwepo kwa fitna pindi  wachezapo kwenye viwanja vya ugenini amesema ''fitna zipo siwezi kusema hakuna lakini tumepanga kukabiliana nazo .



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Cannavaro:Kwa juhudi zetu tutafuzu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top