728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 08, 2016

    STRAIKA WA ARSENAL AENDA KUJARIBU ZALI CHAMPIONSHIP


    London,Uingereza.

    STRAIKA wa zamani wa Arsenal,Nicklas Bendtner,amejiunga na klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi daraja la kwa England maarufu kama Championship.

    Bendtner,28,amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Nottingham Forest baada ya kutemwa na klabu yake ya zamani ya VFL Wolfsburg ya Ujerumani aliyojiunga nayo kwa uhamisho wa kudumu mwaka 2014.

    Baada ya kusaini mkataba huo,Bendtner,ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa hajajiunga na Nottingham Forest kwa ajili ya kupata pesa za haraka haraka bali aweze kufurahia soka yake.


    Bendtner amekaa katika klabu ya Arsenal kwa kipindi cha miaka tisa akifunga mabao 47 katika michezo 171 ya michuano mbalimbali.

    Kabla ya kutua Nottingham Forest,Bendtner,pia aliwahi kuchezea vilabu vya Birmingham,Sunderland na Juventus.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STRAIKA WA ARSENAL AENDA KUJARIBU ZALI CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top