728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    VODACOM KUKABIDHI MWEZI UJAO ZAWADI ZA UBINGWA LIGI KUU BARA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na timu nyingine zilizoshiriki katika msimu
    ulioisha wa 2015/2016 zitakabidhiwa zawadi zao mapema mwezi ujao na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

    Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema kuwa ucheleweshaji wa kutoa zawadi hizo baada ya kumalizika,umetokana na baadhi ya timu zinazoshiriki kwenye mechi za mashindano ya kimataifa kama vile mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kuingia kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

    “Tunaomba radhi kwa timu husika,wachezaji na wadau wa soka kwa zoezi hili kuchelewa ila tunawahakikishia kuwa zawadi ziko tayari na zitakabidhiwa mwezi ujao,” alisema Nkurlu.

    Pia alishukuru wadau wote waliofanikisha ligi hiyo hadi kufikia mwisho ambapo Young Africans ya jijini
    Dar es Salaam iliibuka tena bingwa kwa mwaka huu.

    “Licha ya changamoto zinazoendeleza kujitokeza katika ligi yapo mafanikio makubwa na ligi hii inazidi kuwa na msisimko mkubwa nchini tunawashukuru wadau wote na tuna imani kuwa itazidi kuwa bora katika siku za usoni,”alisisitiza Nkurlu.

    Alisema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa udhamini wa ligi hii hata katika msimu ujao kwa mujibu wa mkataba wake na TFF na aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi hii ikiwemo kuwawezesha wachezaji kunufaika zaidi katika ushiriki wake.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VODACOM KUKABIDHI MWEZI UJAO ZAWADI ZA UBINGWA LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top