728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    KOCHA BRAZIL AHOFIA KIFO

    California, Marekani.

    KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Brazil,Carlos Dunga ameibuka na kusema kuwa haofii kutimuliwa wadhifa wake huo baada ya timu hiyo kutupwa nje ya michuano ya Copa America Centenario kufuatia kufungwa bao 1-0 na Peru Jumatatu alfajiri na badala yake hofu yake kubwa ni kifo peke yake.

    Akiongea muda mfupi baada ya kuisha kwa mchezo huo wa Kundi B, Dunga aliyewahi kufukuwa wazifa huo mwaka 2010 kabla ya kurejeshwa tena mwaka 2014 amesema “Rais wa shirikisho la soka la Brazil anajua tunachokifanya na jinsi tunavyofanya kazi.

    "Unapoifundisha timu ya taifa ya Brazil tegemea kukosolewa/kusakamwa sana pindi matokeo yanapokuwa mabaya,lakini ndani tunajua nini tunakifanya.

    “Wabrazil tunataka kila kitu kibadilike ndani ya dakika mbili lakini katika mpira hilo halipo tunahitaji kuwa na subira.Sihofii kufukuzwa,nahofia kifo peke yake".Alimaliza Dunga.

    Brazil ambao ni mabingwa mara nane wa Copa America,Jumatatu alfajiri walitupwa nje ya michuano hiyo baada ya Raul Riudiuz kuifungia Peru bao la utata dakika ya 75 na kufanya mchezo uishe kwa Peru kushinda kwa bao 1-0.

    Kutoka kundi B timu zilizofuzu robo fainali ni Peru na Ecuador huku Brazil na Haiti zikiaga

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA BRAZIL AHOFIA KIFO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top