728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    KAPOMBE KUREJEA SIMBA SC KWA DAU LA KUELEWEKA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Klabu ya Simba imeanzisha shambulizi
    kubwa la usajili linalolenga kumrejesha kwenye kikosi beki wao mahiri wa zamani,Shomari Kapombe, ambaye kwa sasa anakipiga Azam FC.

    Habari kutoka ndani ya klabu hiyo ambayo imethibitishwa na moja wa viongozi wa juu (jina linahifadhiwa), inasema kuwa Simba imedhamiria kumrudisha beki huyo .

    Chanzo hicho kilisema kuwa, ili kuhakikisha Kapombe anarejea kuvaa jezi nyekundu na nyeupe, wameunda timu ya watu wachache kujaribu kumshawishi.

    Kilisema kuwa klabu hiyo iko tayari kuzama mfukoni na kutoa dau la kueleweka ili kuinasa saini ya beki huyo aliyecheza kwa mafanikio Mtaa wa Msimbazi kabla ya kuondoka.

    “Kuna mipango ya kumrejesha Kapombe,lakini siyo kila kiongozi atahusishwa kwenye mpango huu kama ambavyo imekuwa kawaida,” alisema mtoa habari huyo.

    Alisema kuwa klabu hiyo imetenga Sh.milioni 250 kwa ajili ya kujenga upya kikosi chao kilichofikisha misimu minne bila kutwaa ubingwa, huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni usajili mbovu wa wachezaji.

    Alisema lengo la Simba siyo tu kumrejesha Kapombe, bali kusajili wachezaji wenye sifa ya kuvaa jezi zenye nembo ya klabu hiyo.

    “Msimu hakuna makosa katika usajili, kama kulikuwa na makosa, basi tumejifunza.Tunataka kujenga kikosi imara kitakachorejesha heshima ya Simba,”aliongeza.

    Mapema wiki iliyopita, Msemaji wa Simba Haji Marana alisema kuwa mkakati wao wa sasa ni kufanya usajili kimya kimya ili kuepuka ushindaji usio na tija wa kugombea wachezaji kama ambavyo imewahi kutokea misimu ya nyuma.

    Hata hivyo, kuna taarifa kuwa Wekundu hao wa Msimbazi wameshawakamata mezani na kumalizana nao wachezaji kama Emmanuel Semwanza, Malika Ndeule,Mdhamiru Yassin na Jamal Mnyate

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KAPOMBE KUREJEA SIMBA SC KWA DAU LA KUELEWEKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top