728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 13, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JIONI YA LEO JUNI 13,2016

    Jaap Stam

    Stam:Reading imemtangaza beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam kuwa Kocha wake Mkuu mpya.Stam,43 amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kuwanoa miamba hao wa Madejski Stadium.Akiwa na Manchester United,Stam alicheza michezo 127 akipoteza michezo 17 pekee.

    Arnautovic:Stoke City imeamua kumpiga bei kwa shingo upande mshambuliaji wake mtukutu Marko Arnautovic baada ya staa huyo wa Australia mwenye miaka 27 kukataa kusaini mkataba mpya akishinikiza kutimkia katika vilabu vinavyoshika nafasi sita za juu England.(Daily Mirror)

    Feghouli:West Ham United imeripotiwa kuwa karibu kuinasa saini ya kiungo wa Valencia Sofiane Feghouli hii ni baada ya mkali huyo toka Algeria kukubali kuingua kandarasi ya miaka mitatu wa kuitumikia miamba hiyo ya London.(L'Equipe)

    Fabinho:Manchester United na Barcelona zimeungana na Napoli kuisaka saini ya beki wa kulia wa Monaco Fabinho,23.(gianlucadimarzio)

    Koulibaly:Chelsea imepania kuusuka upya ukuta wake hii ni baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £24m ili kumsajili beki wa kati wa Napoli Msenegal Kalidoi Koulibaly,23.(Gazzetta dello Sport)

    Zielinski:Liverpool imetuma ofa ya £9.5 kwenda Udinese kwa ajili ya kumsajili winga wa Poland Piotr Zielinski hii ni baada ya nyota huyo mwenye miaka 22 kukataa kujiunga na Napoli.

    Sobhi:Stoke City imeripotiwa kuwa karibu kuinasa saini ya kiungo wa Al Ahly ya Misri,Ramadan Sobhi,19, baada ya kuvibwaga vilabu vya Arsenal na Roma.

    Valencia:Galatasaray inajiandaa kufungua mazungumzo na winga wa Manchester United Antonio Valencia ili kuangalia uwezekano wa kumsajili katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.(Fanatik)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JIONI YA LEO JUNI 13,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top