728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    HATIMAYE EVERTON YAPATA KOCHA MPYA

    Liverpool, England.

    BAADA ya wiki kadhaa za mazungumzo hatimaye Everton leo imemtangaza Mholanzi Ronald Koeman kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya Muhispania Roberto Martinez aliyetupiwa virago mwezi Mei.

    Koeman,54,amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuwanoa wakali hao wa Goodson Park baada ya waajiri wake wa zamani klabu ya Southampton kukubali kupokea £5m kama fidia ya kuvunja mkataba wake uliokuwa umebakisha mwaka mmoja kufikia ukingoni.

    Uteuzi huo wa Koeman pia utashuhudia kaka wa kocha huyo Erwin Koeman na kocha wa viungo Jan Kluitenberg nao wakiwa sehemu ya benchi la ufundi katika klabu hiyo ya Goodison Park.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE EVERTON YAPATA KOCHA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top