728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    CHELSEA,MAN UNITED CHALI,PJANIC ASAINI JUVENTUS

    Turin,Italia.

    MABINGWA wa Italia Juventus wamevibwaga vilabu vya Chelsea na Manchester United baada ya kufanikiwa kumsajili aliyekuwa kiungo wa AS Roma, Mbosnia Miralem Pjanic kwa dau la Euro 32m ($36.14 million).

    Pjanic,26, amesaini kandarasi ya miaka mitano ya kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Turin baada ya kufuzu vipimo vya afya siku ya Jana.

    Pjanic alijiunga na AS Roma mwaka 2011 akitokea Olympique Lyonnais ya Ufaransa kwa ada ya Paundi 5.3milioni.Akiwa na AS Roma,Pjanic alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 185 akifunga mabao 30 na kutengeneza 46.

    Inasemekana Pjanic ndiye kiungo bora zaidi mchezeshaji kwa sasa Italia katika kipindi cha misimu miwili iliyopita.Pia ni mtaalamu wa kupiga mipira ya adhabu/faulo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA,MAN UNITED CHALI,PJANIC ASAINI JUVENTUS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top