728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, November 08, 2015

    USAJILI:CHELSEA YAMGEUKIA CHICHARITO,LIVERPOOL YAKARIBIA KUMNASA PATO,JANUZAJ KURUDI MAN UNITED,VALDES ANATIA HURUMA

    Na Paul Manjale

    Gaitan:Manchester City imeripotiwa kuwa mbele ya vilabu vya Arsenal,Liverpool na Manchester United katika mbio za kumuwania winga wa Benfica Nicolas Gaitan mwenye thamani ya £24m.(Daily Mirror)

    Pato:Liverpool imefikia makubaliano ya awali na Corinthians kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Alexandre Pato, 26 aliyewahi pia kukipiga na AC Milan ya Italia.(London Evening Standard)

    Saponara:Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kukiongezea makali kikosi chake hapo mwezi januari kwa kumsajili kiungo wa Empoli Riccardo Saponara anayekadiriwa kuwa na thamani ya £14m.(Tuttosport)

    Valdes:Hali ya mlinda mlango Victor Valdes ndani ya Manchester United imezidi kuwa mbaya baada nyota huyo wa zamani wa FC Barcelona kuambiwa akae mbali na kikosi cha kwanza pamoja na kile cha wachezaji wa akiba.(Sun on Monday)

    Ivanovic:Mlinzi wa Chelsea Mserbia Branislav Ivanovic,31 huenda akaihama klabu hiyo majira yajayo ya joto na kujiunga na Inter Milan baada ya kuripotiwa kutakiwa kwa nguvu zote na kocha Roberto Mancini pindi mkataba wake utakapofika kikomo mwezi julai.(Daily Mirror)

    Chicharito:Chelsea imeripotiwa kutaka kuimarisha kikosi chake kwa kufanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez ambaye kwasasa anakipiga na Bayer Leverkusen.Msimu huu Hernandez amefunga magoli 12 katika michezo 19 akiwa na Bayer Leverkusen pamoja na Mexico wakati Chelsea imefunga magoli 16 katika michezo 12.(Sunday People)

    Simeone:Diego Simeone ameviweka mkao wa kula vilabu vya ligi kuu England baada ya kuripotiwa kuwa yuko mbioni kuiacha Atletico Madrid katika majira yajayo ya joto.Simeone,45 kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa kutakiwa na Chelsea.(Sunday People)

    Willian:Chelsea inapambana vikali kumpa mkataba mpya nyota wake Willian baada ya ripoti kuibuka kuwa vilabu vya Paris Saint-Germain na Bayern Munich vimeanza kumtupia macho.(Sun on Sunday)

    Januzaj:Manchester United inafikiria kukatisha uhamisho wa mkopo wa nyota wake Adinan Januzaj katika klabu ya Borussia Dortmund baada ya kutoridhishwa na maendeleo yake katika klabu hiyo ya Ujerumani.Januzaj ameanza katika michezo miwili pekee katika michezo tisa aliyocheza.(Sunday Mirror)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:CHELSEA YAMGEUKIA CHICHARITO,LIVERPOOL YAKARIBIA KUMNASA PATO,JANUZAJ KURUDI MAN UNITED,VALDES ANATIA HURUMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top